
ENDELEA....... "Mbona unaongea ni kama vile umefanya jambo la kawaida na wala hujutii makosa yako. Vipi unafikilia nini kuhusu familia na ukoo wetu? Huoni kama umetusababishia laana?" "Ni jambo la bahati mbaya" "Mbona kama ni bahati mbaya unajali sana kuhusu yeye. Imefikia hatua unanipiga na wala haunisikilizi kwa chochote wala kujali kuhusu mimi" "Ni kwaajili ya mtoto tu ila tambua wewe ndiyo mwanamke wa maisha yangu" "Ni Upuuzi mtupu" niliongea hayo kwa hasira niliinuka nikataka kuondoka ila Sony alinidaka mkono wangu. Muda huo huo Manka alifika eneo hilo. Taratibu Sony aliniachia mkono ndipo nikajua kwa sasa Manka ndiye udhaifu wake.
0 Comments