Klabu ya Simba imezoa tuzo zote kwenye Kombe la Muungano 2026

Klabu ya Simba imezoa tuzo zote kwenye Kombe la Muungano 2026

ambapo tuzo ya mchezaji bora wa mashindano imekwenda kwa beki wa kati, Rushine De Reuk huku mfungaji wa bao la ushindi Selemani Mwalimu 'Gomez' akitwaa tuzo ya mfungaji bora akiwa na magoli matatu. Kocha wa Simba SC, Steve Barker ametwaa tuzo ya kocha bora wa mashindano huku tuzo ya mchezaji bora chipukizi ikichukuliwa na kinda wa miaka 15, Hussein Ally Mbegu wakati Hussein Abel akitwaa tuzo ya golikipa bora wa mashindano ya Muungano Cup 2026. Simba SC imetwaa Kombe la Muungano kwa mara ya saba na kuifikia Yanga SC ambayo pia imetwaa Kombe hilo mara 7. FT: Yanga SC 0-1

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments