
Walishuka ngazi na kukimbilia eneo la nyuma la bustani ambako taa zilikuwa hazimuliki vizuri. Walinzi wawili wenye tochi kubwa walikuwa wamesimama karibu na kichaka kimoja kikubwa cha maua ya waridi, wakimulika chini. "Kuna nini hapa?!" Mzee Salim alifoka, akielekea pale huku bastola yake ikiwa imenyoshwa mbele. "Bosi, tumemkuta hapa... lakini hajatupinga. Alikuwa tayari ameshadhoofika sana na alikuwa anajivuta chini kwa shida," mlinzi mmoja alieleza. Mwanga wa tochi ulidondoka juu ya kiumbe kilichokuwa kimejilaza chini kwenye matope. Alikuwa ni Bi. Biashara. Lakini hali yake usiku huo ilikuwa ya kusikitisha mno kuliko alivyokuwa hospitalini. Nguo zake zilikuwa zimechanika kwa miiba ya uzio,
0 Comments