
Mwili wa Bi. Biashara uliobaki baridi kwenye matope ya bustani ulikuwa kama shahidi wa mwisho wa ukuta wa uongo ulioporomoka usiku huo. Mvua iliyokuwa imekatika ilianza tena kwa manyunyu madogo madogo ya baridi, ikisafisha damu iliyokuwa imetapakaa kwenye kanzu nyeupe ya Ayman na kwenye mikono ya Mzee Salim. Mzee Salim alikuwa bado amepiga magoti, macho yake yakitazama chini kwenye matope bila kupepesa. Bastola yake ilikuwa imelala pembeni yake, ikiwa imepoteza nguvu na maana yake yote. Kila kitu alichokipigania, kila kiburi alichokuwa nacho kwa miaka hamsini ya maisha yake, na kila dharau alizowahi kuwamwagia masikini wa jiji la Dar es Salaam—kumbe
0 Comments