
SEHEMU YA 11 Milio ya mashine za chumba cha dharura ilianza kubadilika na kuwa ya kasi, ikionyesha mapigo ya moyo ya Ayman yalikuwa yanashuka kwa kasi ya kutisha. Daktari mkuu aliwasukuma Mzee Salim na Mama Amina kwa dharura. "Mzee Salim, simama! Kama unataka mwanao aishi ili umwombe msamaha, lazima tuingize damu yako mwilini mwake sasa hivi! Kila sekunde inayopotea inamvuta kaburini!" Mzee Salim alifuta machozi yake haraka, akajikaza na kulala kwenye kitanda cha dharura kilichokuwa jirani na cha Ayman. Muuguzi bingwa aliunganisha mipira maalum, na damu ile ya O-Negative ilianza kutiririka kutoka kwenye mshipa wa Mzee Salim kwenda mwilini mwa
0 Comments