
SEHEMU YA 1 " Mtoto mvivu wewe khaaa !!! siamini kama tangia asubuhi nimekuacha ndo vile nilivyokukuta, si nguo si kuoga wala sebule ni hivi hivi....ama kweli wenzangu wanazaa ila hapa nilijisaidia hakika " alizungumza mama yangu huyo bibi cha mdomo pindi alipotia mguu wake nyumbani kwetu. " Nipo kwenye siku zangu mama hakuna hata kazi niwezayo kuimudu.. maumivu niyasikiayo ni balaa " nilizungumza. " Kula, kunywa kulala, kujibizana na mama yako ndo kitu pekee unaweza sio ? " "Lakini mama ? " " Sina haja ya kuongea mara mbili " alizungumza mama kisha akanikata jicho la mwana ukome 😀,
0 Comments