
(1) ELEWA KWANZA FREELANCING NI NINI Freelancing ni kufanya kazi kwa wateja kupitia mtandao na kulipwa kwa kazi unayofanya, si kwa kuajiriwa ofisini. Unaweza kufanya kazi ukiwa nyumbani, kijijini au mjini, mradi una simu au kompyuta na intaneti. Hakuna uchawi wala miujiza. Ni kazi halali kama kazi nyingine zote, tofauti ni kwamba unajitegemea. Inahitaji muda, subira na kujifunza hatua kwa hatua, si kukurupuka. (2) FAHAMU WEBSITE ZA KAZI ZA MTANDAONI Kuna website maalum zinazounganisha wateja wanaohitaji kazi na watu wanaojua kufanya kazi hizo. Hizi website ndizo msingi wa freelancing. Ndani yake, mteja anaweka kazi, na wewe unaomba au unaweka huduma
0 Comments