
Nilihisi kama sijaona vizuri, nikaanza kumuangalia kwa makini sana ni kweli alikuwa ni yeye, cheka yake, na namna ambavyo anaongea, dimpoz zake, urefu wake yaan kila kitu alikuwa ni yeye, ila tofauti ni kwamba alikuwa na afya na amenawiri sana.. Nikaja kushtuliwa na harufu ya vitunguu kuunguwa ndio nikashtuka na kuanza kupika upya… Nilikuwa sielewi kabisa kama ni nina ota au laa, maana kila kitu yaan kitu alikuwa sawa sawa na omari, sasa kichwan kwangu nikawa na majibu na maswali kadhaa, la kwanza, huenda labda wamefanana tu maana duniani watu wawili wawili, na kingine kama angekuwa ni yeye si angerudi
0 Comments