
"Fredy, nini kuvutana bana!" Sada aliongea kwa maumivu mkononi... "Sada, nisikilize: tabia ya kumpiga Kasie bila kosa lolote acha! Kuna siku utakuja umpige upate balaa!" Fredy alilalamika... "Khaaaa! 😆 Nicheke ninenepe mie! Kwanza huyo Kasie nimpige mimi wa umri wangu huu? Halafu tena, kama ningempiga wala asingesema lakini hajapigwa analeta shobo," Sada aliongea akiwa anautikisa mwili wake. "Shenzi (Fredy alimtwika kibao da Sada), pumbavu wewe! Nisikilize: nikirudia kusikia umempiga Kesie utaujua undani wangu upoje," Fredy aligeuka akitaka kuondoka... Lakini na mimi nilimuwahi nikamuweka mtama kama alivyomuweka da Sada. "Ukome kabisa! Da Sada, twende ndani!" nilimshika mkono da Sada tukaingia ndani.
0 Comments