
Mwandishi;lissa mwalla Nilishangaa mm huyo naitwa mdogo wangu leo na waoo juu😂kweli dunia duara, niligeuka akanikumbatia alikua na wadada wawili neema alikua amechoka mnoo amebeba na mtoto mdogo mgongoni mtoto kajaa kamasi nzito nzito na vumbi, yy mwenyewe kavaa nguo kuu kuu hata kitenge alichobebea mtoto kimechakaa, nilikumbuka alivokua ananifanyia nilitamani nimsukume lkn nikasema ngoja nijikaze. Akaniachia afu akasema pole na safari, nikasema asante, akasema mlifika usiku ee? Nimeshangaa nakuona makaburini, nikasema ndio. Akasema twende ukamsalimie mama yupo kule kwa shangazi juu. Nikasema sawa japo nilitaka nioge kabisa. Akasema basi kaoge kwanza. Nikasema sawa akachukua begi nililobeba et ananibea tukaanza
0 Comments