
Naitwa Radhia, nina umri wa miaka 24. Maisha yangu hayakuwa rahisi, lakini nilijifunza mapema kuwa mwanamke asiye na mtu wa kumtetea lazima ajitetee mwenyewe. Nilihitimu masomo yangu ya Secretarial, nikiwa na ndoto moja tu—kupata kazi itakayoniokoa mimi na familia yangu. Siku hiyo niliivaa suti yangu nyeusi niliyoinunua kwa mkopo, viatu vya kisigino nilivyovumilia maumivu, nikajipaka tabasamu la uongo mbele ya kioo. “Radhia, leo maisha yako yanabadilika,” nilijiambia. Nilikuwa nimeitwa kwenye interview katika kampuni kubwa jijini Dar es Salaam — K-MAX HOLDINGS LTD. Ndani ya jengo la kifahari, nilihisi udogo wangu. Wafanyakazi walionekana kujiamini, wanawake waliongea kwa sauti za uhakika, wanaume
0 Comments