
Tulipoishia... Basi Da Joan tukakubaliana niliishi nae vizuri kipindi niko nyumbani na alikuwa akinipenda sana.. Siku iliyofuata alinitumia msg Akaniambia ndio najiandaa niende kwenu sasa hivi niombee tu baba yako nisimkute ... Kweli alienda mpaka nyumbani kwetu akafika akanipigia kuniuliza sehemu anakoweza kuvipata hivyo vyeti.. Yani nilikuwa hadi natetemeka sijui uoga sijui kitu gani niliomba sana Mungu asaidie Da Joan avipate hivyo vyeti na afanikiwe kuondoka navyo salama.. Nilimwelekeza Da Joan sehemu vilipokuwa vinatunzwa vyeti vyetu akaniambia sawa ngoja nikaangalie.. Alibahatika kuvipata kweli akavichukua na kuvificha..namshukuru Mungu alifanikiwa kutoka salama na vyeti akavikabidhi kwa saji.. Nilifurahi sana.. niliona kama mwanga
0 Comments