
SONGA NAYO.................. Nilibaki namuangalia huku nikijiuliza ana maana gani kusema vile ?,🤔na nitakosaje amani eti kisa kutokuwa karibu yake 🤔na niukaribi gani anaoutaka kutoka kwangu na kwanini atake ukaribu na mimi?.🤔 Niliwaza sana mwisho nikageuka na kuendelea na kazi zangu, dakika zikakata nikamaliza kuandaa vitafunwa bila kupoteza mda nikaandaa meza na kuita wote waliokuwa chumbani . Siku hii madam boss pamoja na aunt Vero walikuwa hawapo hivyo Shuu pamoja na rafiki zake wakasogea mezani Alvin nae hakuwa nyuma . Sasa kwakua huwa siungani nao mezani nikapiga hatua kuelekea jikoni maana huko ndiko ninapopatiaga chakula, ila kabla sijafika Shuu akaniita nami
0 Comments