
MR. AB TULIPOISHIA Piiiiiiiii, alipiga honi konda, nikasogea na kuchungulia vizuri, kweli ilikuwa kama nimetabiri hivi, nilimshuhudia Jerry anashuka kwenye pikipiki amevaa shati na suruali ya kitambaa akasogea “Mke wangu Anita” Alisema Jerry huku akinifuata anikumbatie mimi nimebaki nimeganda kama sanamu sijui nifanyeje. Alinikumbatia ila mimi sikuonyesha ushirikiano maana nilikuwa nina wasiwasi sana akiingia ndani itakuwaje maana atamkuta mwanaume mwenzake. ENDELEA “Mke wangu” Alisema Jerry huku akiwa amenikumbatia “Mbona hauna raha?” aliniuliza na kuniachia akaniangalia usoni mimi machozi yashaanza kunilenga lenga “Et baby” aliuliza na kunifuta machoni kidogo “Why??? Why mume wangu why??” nilimuuliza kwa hasira huku nikiwa natafuta njia
0 Comments