
Nikawa siamini yaani namuona Melvin huyu hapa ila sasa sijaelewa ni kwamba kanisahau au hanikumbuki yaani sijielewi Nikaanza kujifinya nihakikishe kweli sioti nikaona hapana sioti Nikainuka nikamsogelea nikataka kumshika sura ila akawahi kuzuia mkono wangu akaniuliza Wewe dada vipi una shida gani kwani mbona sikuelewi umechanganikiwa Nikasema No Melvin ni mimi Zara ni mimi ina maana hunikumbuki Melvin nilijua ushakufa kumbe upo hai tafadhali niambie ni wewe baba niambie Melvin Yule kaka nikaona anajitoa kwenye mikono yangu maana ni kama alikuwa ananishangaa ikabidi Dick aingilie sasa akanishika mikono akaniambia Mama wawili imekuwaje kwani Nikasema Dick huyu ni Melvin huyu ni
0 Comments