PART 3: MTI UNAOMWAGIKA DAMU

PART 3: MTI UNAOMWAGIKA DAMU

PART 3: MTI UNAOMWAGIKA DAMU Mwandamo usiku ule hakulala mapema. Alifungua mlango na kutoka nje hadi karibu na ule mti. Alichokiona kilikuwa kinatisha sana. Alimuona mwanamke aliyelowa damu huku akilia. Taswira ya yule mwanamke haikumjia vizuri kutokana na mwanga hafifu wa giza. Mwandamo alimtazama tu kutoka sehemu alipojificha. Yule mwanamke alikuwa akivuja damu Kila sehemu. Mwandamo hakuona mti usiku ule ila yule mwanamke anayevuja damu. Aliamua kurudi nyumbani na asubuhi yake akamweleza mama yake juu ya kile alichokiona. "Mjinga wewe, nani aliyekwambia uende? Ule mti umeraaniwa. Acha kuusogelea" Aliongea mama yake. Siku hiyo mwenyekiti aliitisha mkutano na wanakijiji wote walikusanyika.

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments