
PART 5: MTI UNAOMWAGIKA DAMU Mwenyekiti na wazee wachache wa kijiji walifika kwenye ule mti wakiwa na Mbuzi mweupe. Mganga alimchinja yule mbuzi na damu yake kuielekeza kwenye ule mti. Alichukua dawa yake na kuinyunyuzia sehemu yenye damu na Kisha alianza kuongea na miungu. Damu haikukata badala yake iliongezeka. Usiku wa siku hii sauti ya mwanamke akilia ilikuwa kubwa zaidi. Hofu ikatanda tena. Mwandamo kama kawaida yake. Mawazo mengi kichwani. Usiku ule aliwaza sana. Alimuwaza yule mwanamke anayeomba msahada. Aliwaza kitu kipi kinamfanya awe pale akiteseka. Ingawa mama yake humzuia kwenda kwenye ule mti lakini safari hii lilimpata jambo. Usiku
0 Comments