
niahidi utakuwa sawa tu.” Nilikuwa natokwa na machozi nikisema “dada unaongea kama unaniaga vile, hakuna kibaya kitatokea. Utakuwa salama, niahidi utatetea uhai wako.” Dada alitabasamu na kusema “Nakuahidi, sikia mdogo wangu. Nampigia simu shemeji yako, ila hapokei simu yangu. Nenda kwake. Mwambie hali yangu pengine atakuja.” Nilitabasamu na kusema “Usijali, nitafanya hivyo. Sasa jiandae mimi nitakuwa nje nakuombea sitaondoka mpaka ujisikie nafuu.” Dada yangu alitabasamu, aliniambia “nashukuru mdogo wangu nitakuwa sawa.” Nakumbuka nilitoka katika kile chumba nikilia, hata boss wangu aliponiona alinihurumia sana, alikuja na kunikumbatia akisema “totoo, unaweza ukaacha kulia tafadhali. Unapolia unaniweka katika wakati mgumu sana. Moyo wangu
0 Comments