
Nilijisahau kabisa mpaka pale mkuu wa chuo alipompigia baba simu kumwambia sijahudhuria masomo karibia semista mbili nzima. Babal alikasirika sana, akanipigia simu akaniambia nirudi Tanzania mara moja. Niliporudi, maisha yangu yakawa magumu. Baba na mama walinifungia ndani kama mfungwa. Waliniambia hiyo ndiyo adhabu yangu kwa kuwavunjia heshima. Sikuwa na cha kufanya, Nilikaa ndani siku zote, nikichezea simu na kusikiziliza mziki Lakini nilianza kuchoka maana sio siri Nilihisi ninabanwa sana. Nikaanza kukumbuka utamu wa club usiku. Nikasema weeh usinichezee akili, Nilipanga nitoroke usiku wakati wote wamelala, niende club kisha nirudi mapema kabla hawajaamka. Basi Usiku ule, nilingoja wote walale kisha nikatoka
0 Comments