
Maria akiwa bado anafikiria Liya alimwambia " Usijisimamishe Kama mshumaa Kama umeimaliza kuongea na simu njoo ubebe vitu. " Liya unajua sielewi boss Bryan ananiitia Nini " Sasa si uende ukajue unachoitiwa. " Hapana namjua vizuri Sana atanifokea na kuniambia maneno mabaya alafu atanifukuza kazi, Bora nijiachishe mwenyewe. " Basi sawa utatafuta kazi nyingine. Waliendelea kuhamisha vitu Maria akahamia nyumbani kwakina Liya . Malia aliondoka huku akiangalia nyumba yao Nilipenda Sana nyumba yetu, kumbukumbu zangu zote za tangia utoto naziacha hapa . " Imeshatoka hata ukilalamika huwezi kuirudisha kwahiyo kubaliaba na ukweli. " Sawa ,nitafanya kazi Kama punda nipate nyumba
0 Comments