
Jina langu ni Vicky, mke wa mwanaume ninayempenda kuliko nafsi yangu. Nimeolewa na Kelvin kwa miaka mitano sasa. Maisha yetu yalikuwa ya kawaida, si tajiri kupindukia, lakini tulikuwa na furaha yetu. Niliamini ndoa yetu ilikuwa imara… hadi siku nilipoamua kuajiri mfanyakazi wa ndani mpya. Nilikuwa nimechoka kufanya kila kitu peke yangu. Ofisini nachelewa, nikifika nyumbani nashughulika na chakula, kufua, na usafi. Kelvin alikuwa akinishauri mara nyingi: “Mke wangu, tafuta mtu wa kusaidia kazi za ndani… sio lazima uchoke hivi kila siku.” Mwisho wa wiki ile nilipoamua, nilipigiwa simu na jirani yangu akisema anajua msichana mzuri, mpole, na mwenye heshima anayehitaji
0 Comments