
Katika Qur-aan na Hadiyth kumetajwa moto kuonesha mazingira mabaya watakayoshukiwa watu waovu, Waliompinga Allaah na kuendesha maisha yao ya hapa duniani kinyume na kanuni na taratibu alizoziweka Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala). Maisha ya motoni ni kinyume na maisha ya Peponi ambayo picha yake tumeshaiona. Tunafahamishwa katika Qur-aan kuwa motoni kuna Daraja au Milango saba, na kila mlango iko sehemu iliyogawanywa. “Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipoahidiwa wote. Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa”. [Suratu-Al-Hijr:43-44]. Daraja hizi za moto zimepewa majina kama tusomavyo katika Qur-aan: 1️⃣ 𝗝𝗔𝗛𝗔𝗡𝗡𝗔𝗠: Katika Aayah nyingi jina hili limetumiwa, Kama
0 Comments