
taratibu akarudi chumbani kwake , alijikaza kitandani . " Sasa kwanini afanye hivi? Kama kulikuwa hakuna kazi si angeniambia haiwezekani nijue moja ? Lina aliwaza sana mpaka mwisho akafikiria kurudi kwa Mishely ili ampe michingo ya kazi zake. Siku hiyo jioni Jerry alikuwa amekaa bustani huku akinywa kinywaji , Lina alimfuata. " Habari yako boss Jerry alimuangalia kisha akatoa tabasamu dogo. " Salama Lina, karibu ukae. Lina alikaa kwenye kiti cha pembeni yake . " Samahani naweza kuongea na wewe? " Bila shaka unaweza. " Siku ile tukiongeza kuhusu kazi lakini hukuniambia mshahara wangu utakuwa kiasi gani? Jerry alimuangalia kisha
0 Comments