
" Ni kweli sijafika kuna mambo yaliingiliana. Mishely alikunja uso wake. " Unamaana gani kunijibu hivyo? Kwahiyo hayo mambo yako yaliyoingiliana yalikuwa muhimu sana kuliko hilo lililokupeleka? " Mishely sijui nikwambiaje ili unielewe maana mimi mwenyewe hapa nilipo ni kama nimechanganyikiwa. Nilienda mpaka kwenye chumba cha mr Jovin wakati nataka kugonga mlango alikuja mwanaume mwingine na kunipeleka kwenye chumba cha Jerryson yule billionea kijana ambae alipata tuzo mwezi uliopita na kuonyeshwa sana kwenye TV. Mishely alikuwa ana muelewa vizuri sana Jerryson alitoa macho kwa mshangao. " Unasemaje Lina? Unamaanisha ulienda kuonana na Double J? " Ndio Nilichukulia nikaenda kuonana na
0 Comments