
Kusamehe haraka hivo kwangu ni Big noo mpaka nihakikishe umeteseka na umejifunza ndo nitakusamehe.. Hizo za umekosea jana leo nakusamehe huo ujinga sifanyi😒😒😒hizo misamaha ya hara haraka utasamehewa na mamako siyo mimi.. Hayo niliyawaza kimoyomoyo na muda huo Rouhy alikuwa ananibembeleza nimsamehe lakini haikuwezekana... Nilimwambia aendelee kula ujana siku akitosheka mengine yataendelea... Yani nikusamehe kirahisi kesho ukachiti tena😒😒huu msamaha utauhangaikia miaka na miaka mshenzi wewe😒 Rouhy alivoona msamaha imeshindikana alinirudishia simu ila akaniomba nisimwambie yeyote kuhusu kilichotokea.. Nilimkwapua tu simu nikamuacha aongee na hewa huko chumbani😒 alikaa huko chumbani akawaza weee baada ya hapo akaenda Jikon akakuta chakula alichonipikia asubuhi
0 Comments