
Kelvin alifika kwenye geti la Maramba Secondary School asubuhi yenye upepo mzuri wa bahari, akiwahisi wanafunzi wakipita pembeni yake wakiwa wamevalia sare zao za kijani na kahawia. Akiwa amejawa na matumaini na hamu ya kuanza kazi yake mpya, aliendelea mbele hadi ofisi ya mkuu wa shule, ambapo alipokelewa kwa tabasamu na Mwalimu Samuel, mkuu wa shule. Mwalimu Samuel alimkaribisha Kelvin rasmi, akimwonyesha maeneo muhimu ya shule hiyo na kumweleza taratibu zote za Maramba. Asubuhi hiyo ilipofika saa 1:30, kengere iligongwa na wanafunzi walikusanyika uwanjani kwa ibada ya asubuhi. Baada ya salamu rasmi, Kelvin alipata nafasi ya kujitambulisha mbele ya wanafunzi.
0 Comments