
Polepole nikaanza kugundua kitu cha ajabu. Kila usiku, analala na nguo zake za kawaida za kulalia. Lakini saa sita kamili za usiku, nilimkuta amesimama akiwa na gauni jekundu. Asubuhi ikifika… unamkuta amevaa nguo zake za kawaida. Usiku wa kwanza nilipuuza. Usiku wa pili nikajisemea ni bahati mbaya. Lakini ulipofika usiku wa tatu, nilijua kabisa hili sio kosa wala mzaha. Na muda mwingine… hata kitandani hakuwapo kabisa. Asubuhi moja nikamuuliza.. “Mpenzi, mbona kuna wakati nakukuta umevaa gauni jekundu usiku, lakini asubuhi unakuwa na nguo zingine? Kwa nini unabadilisha?” Aliganda kwa sekunde, kisha akacheka taratibu… “Mimi? Gauni jekundu? Acha mpenzi. Unajisumbua bure.
0 Comments