
13 Nadia alishindwa kuendelea kukaa pale ofisini alinyanyuka na kutoka huku kabir akiwa anamsindikiza kwa macho na kusahau kama Jayden yupo pale. " Vipi kuna tatizo? Jayden aliuliza " Hapana. Jayden valimuonyesha sehemu ya kusain kisha akatoka na kuelekea moja kwa moja ofisini kwa Nadia. " Vipi Nadia kuna jambo lina kusumbua? " Hapana. " Unajua haipaswi kujificha kitu Nadia. " Naomba uniachie nataka kukaa pekee yangu . " Kuna kitu kinaendelea kati yako na kabir na ndio maana siku ile kwenye sherehe ulikuwa huna amani hata kidogo. Nadia hakuwa na cha kujitetea alinyamaza kimnya. " Una uhusiano nae kimapenzi?
0 Comments