
Kabir alitamani kuongea kitu lakini Nadia alikuwa na hasira sana, Amina rafiki yake Nadia alimuangalia sana kabir kama vile alikuwa anataka kuuliza kitu. Kabir aligundua hilo taratibu aliondoka kwenye lile eneo akaenda chumbani kwake. " Nadia naomba usilie , hebu twende ukapumzike. Amina alimshika mkono wakaenda chumbani Nadia alisimama pembeni ya mlango wa chumba chake, moyo wake ukiwa bado na huzuni. Rafiki yake, Amina, aliiona uso wake uliokuwa umejaa huzuni na macho yaliyochoka. " Nadia utakuwa na njaa nikakuletee chakula? " Hapana sina njaa. "Mbona unaonekana kuchoka na midomo imekaukia hata uso wako kama una huzuni , nini kimekupata huko
0 Comments