MIMBA YA DHARURA 4

MIMBA YA DHARURA 4

Nadia alijifungia chumbani kwake, moyo wake ukiwa na shauku ya kutaka kujua kwenye ile barua kimetandikwa nini. Alipofika alichukua begi lake akatoa ile barua alikaa kitandani akafungua ile barua na kuangalia macho yake yalikuwa na hofu pia alikuwa na hamu ya kujua yaliyomo. Kwa sekunde kadhaa aliitazama tu, alishusha pumzi kwa nguvu kisha Akaanza kusoma: "Nadia, Samahani kwa kile kilichotokea. Najua nilikuvunja, niliharibu kitu kisichostahili kuharibiwa ila ni maalumu kwa mtu aliyedhamiria kufanya hivyo. na kila dakika inayopita moyo wangu unaniuma zaidi Sikukusudia. Usidhani kuwa nilikuchukulia kama mwanamke wa kawaida, la hasha, wewe ni tofauti, ni wa thamani kubwa zaidi.

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments