
Siku ile haikuwa ya kawaida kwa Nadia. alikuwa na matumaini makubwa ya kufanikiwa alikuwa na imani anaenda kutafuta mwanga mpya wa maisha yake na ya mwanawe. Akitoka na kuchukua usafiri wa pikipiki ukampekeka mpaka kwenye kampuni moja ya simu. Alishika kwenye pikipiki akasimama huku akiangalia lile jengo huku akiomba dua aweze kupata kazi baada ya kuzunguka na vyeti vyake kwa muda na bila mafanikio. Alipiga hatua kwa ujasiri japokuwa ndani yake hofu ilimtafuna. Alijipa moyo kwa kusema “Usiogope Nadia kumbuka unatafuta riziki sio kwa ajili yako peke yako bali kwa ajili ya malaika wako mdogo. Hii ni hatua ya mwanzo.
0 Comments