
Macho ya Leon na Jasmine yalikuwa yamefungwa kana kwamba kuna sumaku iliyokuwa ikivutana. Pumzi zao zilikutana, joto la miili yao likawa karibu mno. Leon alinyosha mkono wake kana kwamba anataka kugusa shavu la Jasmine, lakini kabla hajafanya hivyo mlango ulifunguliwa kwa kwa nguvu na kufanya washituke na kila mtu akarudi nyuma. “ samahani Boss!” alijitokeza Paul, mmoja wa wafanyakazi wa kampuni . Leon alimuangalia huku akiwa kakunja sura yake . “Samahani, kuna dharura ya mikataba inahitaji sahihi yako haraka. Kwa sauti kali Leon alijibu: “Paul! Wewe huna adabu? Huoni niko busy? Toka nje nitakuita! " Samahani boss... Paul alijifuta jasho,
0 Comments