
12 Doreen alishuka kwenye ngazi taratibu na kuwafuata waliposimama. "Bravo! Bravo! Naona mpo kwenye mambo yenu. Doreen alisema kwa sauti ya dhihaka. Kwani ilikuwa inahitaji mpaka niwaone ili niamini? Sasa nimeamini! Damian, kumbe hiki ndicho unachokifanya ukiwa nyuma ya mgongo wangu?" "Doreen si kama unavyofikiri......" Damian alijaribu kujitetea lakini Doreen alimpungia mkono akimkatisha. "Acha hizo! Vanessa si alisema? Alisema wazi kuwa anapigania nafasi yake, na leo nimemwona akijaribu kuchukua nafasi hiyo kwa vitendo. Kwa kweli hongereni , hongereni sana . Vanessa alisimama kwa utulivu lakini macho yake yalikuwa makali na ya kujiamini. "Kama ulikuwa na mashaka, leo umepata jibu. Lakini
0 Comments