
"Heeeee hii imekuwaje tena!? Mbona kama naota!?" Jovin akiwa anaugulia maumivu alijiuliza swali ambalo hata hivyo hakupata majibu ya haraka haraka!. Jovin aliondoka pale akiwa anajiuliza maswali mengi ambayo hayana majibu sahihi!. Ilipo fika Jioni Jovin aliamua kumfuata yule Mr Antonio nyumbani kwake Ili kuuliza Nini kinaendelea, ni kweli alimkuta bwana huyo katulia na familia Yake!. "Mr Jovin Mimi nafuata maagizo ya boss, huu ni ujinga Wako na uzembe wako! Wazo lako la kujifanya na kuigiza umasikini nadhani unaenda kuwa masikini kweli!, naomba uondoke Mimi sina cha kukusaidia na kaa ukijua, mkurugenzi Wa *JovinMotor Company* kwa Sasa ni Mr Tamir!"
0 Comments