MY CRAZY HOUSE GIRL* *______________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*

MY CRAZY HOUSE GIRL* *______________________________________*  *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*

Asubuhi ilipofika Damian alikuwa macho siku hiyo hakulala usingizi mzuri Alikuwa akifikiria makbo anayofanya Vanessa na licha ya kuwa anamkosea lakini hawezi kumfukuza . " Huyu msichana sijui kampa nini mama inaonekana mama anampenda sana hasikii chochote kutoka kwangu . Ila akiendelea kuniletea ujinga wake nitakifukuza nyumbani kwangu bila kujali chochote hawezi kunipangia jinsi ya kuishi wakati mimi ndio boss hapa. Alinyanyuka pale kitandani na kwenda bafuni kuoga, kisha alivaa suti yake na kushuka chini akaelekea jikoni. Huko alimkuta Vanessa tayari amevaa apron yake, akihangaika na vyombo huku sauti ya muziki wa taratibu ikicheza. Harufu nzuri ya kahawa ilitawala jikoni.

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments