
hakuuachilia kwa haraka aliushikilia kwa muda huku akiwa ananitizama usoni kwangu niliachilia tabasamu ilimradi tu asijisikie mnyonge aliniangalia sana kisha akaniambia asante sana Pink aliniachilia mkono nami nikaanza kuondoka kule ndani kwake kabla sijapiga hatua nyingi Jordan aliniita na kuniomba nisubilie anitoe aliingia chumbani kwake akabadili nguo kisha akatoka na koti zito kalishika mkononi aliniomba nivue ile koti yangu kwani ilikuwa imelowa ilinyeshewa kipindi namsaidia Jordan kule njiani.....Jordan aliniomba nivae ile koti yake nilikubali sikutaka kumfanya ajihisi mnyonge si mnajua watu wenye matatizo huwa wanahitaji faraja eh🙃🙃 nilivaa koti yake ilikuwa inanukia marashi mazuri sana nilimshukuru alinitoa hadi nje kabla
0 Comments