
*________________________________________* *SEHEMU YA 01* (Maalumu kwa Mama wakwe wote wenye viherehere 😅) "Make-up aliyopakwa haijaendana na rangi yake kabisa" "Bwana harusi ni mzuri kuliko Bibi harusi sijui umeiona hiyo" "Sina uhakika kama ndoa yao itadumu, bwana harusi anaonekana kurogwa siyo akili zake hakika... ingekuwa ni akili yake asingeoa Mwanamke wa dizaini hii" Maneno haya yalizungumzwa wakati zoezi la harusi likiendelea, leo ni siku ya furaha kati ya Herman na Salha watu wengi wamehudhuria kwa lengo la kushangaa aina ya Mwanamke aliyemteka Kijana huyu, hivyo wenye roho za kwanini walikuwa bize kukosoa muonekano wa Bibi harusi na si kuwapongeza wanandoa Zawadi
0 Comments