
*__________________________________________* *KUMI NA SITA* Nilipofika pale pale tulipokubaliana na Filex, moyo wangu ulikuwa mchanganyiko wa matumaini na hofu. Nilikuwa nimechoka, lakini bado nikiwa na woga wa kutaka kuamini tena mtu. Kila jambo lilionekana kuwa gumu, kila hatua ilihitaji ujasiri mkubwa, na ndani ya moyo mwangu kulikuwa na kivuli cha mashaka: je, kweli Filex ananipenda? Je, ananihitaji kwa moyo wake wote? Au ni upendo wa msukumo tu wa wakati huu wa matatizo? Tulikaa pamoja chumbani kwake, akinitazama kwa upole na kuonyesha dhati ya huruma na upendo aliyokuwa nayo kwangu. Alinibeba mikononi mwake kwa mkarimu, akaniambia, “Lulu, najua umeumia sana. Najua unahisi
0 Comments