
Nililia mno mpaka nikalala,nilikuja kuamka mchana sim yangu ikiita niliangalia mpigaji alikuwa Khashim nilipokea akaniuliza niko wapi nikamwambia akataka kuja nikakataa na kuamka nikaingia bafuni nikaoga vizuri kisha nikavaa kawaida sikutaka kujifunika wala kujitanda Nilivyoona niko sawa nikatoka na kukuta Jabir amelala kwenye sofa nikampita na kuondoka. Nilienda mpaka hotel moja hivi iliyokuwa karibu na pale nyumbani nikampigia Khashim na kumwambia aje pale, hakuchukua mda akawa amefika cha kwanza alinikumbatia na kuniambia "kwann hukuniambia kama unapitia wakati mgumu namna hii mimi nimekaa huko nikijua uko sawa kumbe sivyo" Kama kawaida nikiulizwa badala ya kujibu naumia na kuanza kulia ndivyo nilifanya
0 Comments