
Saa tatu asubuhi, katika ofisi ya mwanasheria mdogo wa jeshi iliyopo ndani ya kambi ya Lugalo, Giann na Dativa walikuwa wameketi upande mmoja wa meza ya mbao. Mbele yao, palikuwa na karatasi ya mkataba wa ndoa, ulioandaliwa kwa mujibu wa sheria za kijeshi. “Mmekubaliana kufunga ndoa ya kiserikali? Mwanasheria aliwaangalia wote kwa zamu. “Ndio,” walisema wote wawili kwa pamoja, ingawa sauti ya Dativa ilikuwa dhaifu kiasi. Giann alichukua kalamu, akasaini kwa msimamo na ujasiri. Alimwangalia Dativa. “Your turn,” alisema kwa sauti ya upole, lakini yenye heshima. Mikono ya Dativa ilikuwa inatetemeka kidogo aliposhika kalamu. Aliangalia jina lake na nafasi ya
0 Comments