
ENDELEA...... Siku Saba za fungate ziliisha. Asubuhi ya siku ya nane siku hiyo niliamka mapema kwaajili ya kumuandaa Samir kwenda kazini. Cha kwanza kabisa nilimchagulia nguo za kuvaa na baada ya hapo nilizinyoosha. Nilimchagulia viatu na kuviweka katika hali nzuri. Baada ya hapo nilifanya usafi wa chumbani kwangu. Nilienda jikoni nilimkuta mdada wa kazi anapika vitafunwa. Nilisalimiana nae na baada ya hapo nilichemsha maziwa kidogo na kuyabeba kwenye kikombe cha udongo. Niliingia chumbani Samir Bado alikuwa amelala. Niliaangalia saa ya ukutani ilikuwa Unasoma ni saa Moja. Nilianza kujishauri kumuamsha. Nikiwa nawaza naanzaje kumuamsha. Namshika wapi 😅 nilimuona mwenyewe anajigeuza. Haraka
0 Comments