
ENDELEA...... Samira alinitazama Kwa hasira mie Wala sikujali. Alisusa kunywa chai, alienda chumbani kwake. Tuliendelea kunywa chai, baada ya kumaliza kunywa chai mama aliniambia. "Nadra kuwa makini na Samira maana ana makundi ya ovyo sana hashindwi kukujia hapa na kundi lake wakupige". "Mama usijali. Mimi nimekubali kuwa mama Bora na sio bola mama. Nakuhakikishia Samira lazima atabadilika na atakuwa Binti mzuri mwenye maadali. Nilichogundua Samira ukimkazia sauti na kumuonyesha msimamo wako ananywea kama hivyo, atakasirika na kuondoka. "Ni sawa". Mama aliitikia Kwa unyonge alionyesha hofu juu yangu kwasababu anamjua vizuri mjukuu wake. Nilienda jikoni nilimmiminia chai na vitafunwa, nilielekea chumbani
0 Comments