
ENDELEA...... Baada ya kuudaka mkono wa Samir wote walinishangaa. Taratibu nilishusha mkono wa Samir, Samir alikuwa ananiangalia kwa hamaki na Samira alikuwa ametulia nyuma ya mgongo wangu. "I'm sorry". Nilimuomba Samir msamaha. "Tangu lini mwanamke akawa juu ya mwanaume, hii ni ndoa au ndoano". Wifi Najma aliongea hayo. "Kelele na wewe, unaongea Nini?". Mama alimfokea Wifi. "Si unaona lakini anamzuia mumewe kufanya anachotaka. Kuna ndoa hapo mama kama ameanza kudaka mkono wa mumewe". "Baba Samir nisamehe". Nilimuomba Tena msamaha Samir. Samir hakunijibu. Aliondoka kuelekea juu chumbani. "Nisamehe mama". Nilimuomba mama mkwe wangu msamaha, mama alinisogelea na kunishika shavuni kwangu huku
0 Comments