
Niliongea mengi labda nimuelewesha kaka angu lakini ndo kwanza aliniacha naongea akaondoka zake, niliboka nasema we ngoja akupige tukio akili ikusogee vihela vya boda boda vyote mpka pikipiki yenyewe utauza shauri yako. Hata hakunijibu, nilipika zangu mambo yanazidi tu kunichanganya, nilipoingia ndani nilichukua simu nikawa nampigia eliza, we nilipiga mpaka nikakoma hakupokea simu yangu nilitamani kumtumia msg ndefu ila nikasema tutaonana kesho hiyo niongee anaye macho kwa macho. Asubuhi bwana ile nafika chuo kama kawaida nilikuwa na karim, kwa mbali si namuona eliza anashuka kwenye gari ya kibabu chake kimoja aisee nilisikia hasira. Nilitoka haraka mpaka pale nae alikuwa asimamado
0 Comments