
Asante ๐ nilichukua huyo nikaondoka zangu nikamuacha yeye anaendelea kusoma .. Kuna watu wanapenda kusoma mh huyu kaka atakua na akili sana,, mke wake atakuwa na mtu wa maana sana... Nilijisemea moyoni Nilifika nyumbani .. Niliwakuta wenzangu wamekaa wanaangalia TV. Mwenzetu sasa hivi unakaa chuo hadi jioni unatafuta nini? Aggy aliniuliza Nilikuwa najisomea kingine nilienda maktaba ili niazime kitabu... Mh hebu nikione hicho kitabu Penina aliongea huku akinisogelea... Mh mbona unanukia pafyumu tofauti na yako hii si pafyumu ya yule kaka Gerson.. Ulikuwa na Gerson au ๐ค Penina aliniuliza Sikuwa nae mimi nimesema nilienda maktaba nimeazima kitabu nimerudi nyumbani... Angel
0 Comments