VERY HANDSOME 🌸Lover boy💓💓08

VERY HANDSOME    🌸Lover boy💓💓08

Nilikaa na dukuduku langu moyoni ila nikashindwa kumwambia mkaka wa watu asije akaniona muhuni..... Basi tukawa tunajiandaa na mitihani ya semester kila mtu alikuwa bize mara nyingi tukawa tunajadiliana kwenye makundi yetu baada ya hapo kila mtu anaenda kivyake kujisomea... Hatimaye tukafanya mitihani tukawa tumefunga chuo... Nilienda darasani kuchukua begi ili nirudi nyumbani tukajiandae na safari ya kurudi nyumbani Dar nilimkuta Gerson anasoma kitabu... Wewe ndio hutaki kurudi kwenu 😁 nikamtania. Natamani sana nimemkumbuka mama yangu. Ohh hata mimi nimemkumbuka sana.... Sasa si ndio hurudi nyumbani ukamuone. Natamani sana kama angekuwepo but alishafariki muda mrefu sana nimelelewa na shangazi yangu.....

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments