
Mom Lakini Paschal ni Boss wangu na hajawahi kuonyesha kunitaka Mimi nitawezaje Sasa kumshawishi yeye kuwa Karibu na Mimi!?. nilimuuliza Mom Paschal baada ya kuwa ameniomba Mimi niweze kujenga mahusiano ya kimapenzi Kwa mtoto wake! Pendo wewe ni mrembo na pia ni msomi una Kila sifa njema za kupewa mwanamke tumia akili Yako na urembo wako Ili kuweza kumuokoa Mtoto wangu tafadhari Binti yangu nisaidie et Mimi kama mama naumia kumuona Mtoto wangu akiwa anapitia changamoto hizo za kupoteza fahamu Kila mara anapokumbwa na msongo wa mawazo hili tatizo likiwa kubwa nitampoteza kijana wangu sitaki Paschal akutwe na baya lolote
0 Comments