
es Salaam alipokuwa anapoishi.
Meneja wa msanii huyo Abdulrahman Hassan almaarufu Malefti amethitibitisha kifo cha msanii huyo aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia kundi la Tip Top Connection, pamoja na nyimbo ya Nipe Ripoti aliyoshikiana na Tundaman.
Malefti amebainisha kwamba siku ya jana alizungumza na msanii huyo kuhusu mpango wao wa 'kushoot' video ya wimbo mpya kabla ya kuagana saa saba usiku na kubainisha kwamba asubuhi alienda kugongewa kwa ajili ya kutoa nauli za watoto kwenda shule akawa haamki.
Meneja huyo amesema baada ya yaliyotokea majirani walimpeleka hospitali ya Nguvu Kazi iliyopo Chanika ndipo daktari alithibitisha kuwa msanii huyo amefariki Dunia.
Soma zaidi
0 Comments