
BINTI MIA 11 Mwandishi: Chief na simulizi zake WhatsApp: 0621045997 Dokta akaja, hakuwa na maneno mengi. Akatwambia kuwa mama ameshafariki, tufanye utaratibu wa kuwajulisha wakubwa. Basi Victor akaanza nambia, "Si nilikuacha na mama mzima tu anaongea?" Basi nikamwambia umpigie japo baba au shem tuwaambie. Anasema hakumbuki password ya simu na mimi hapo siijui. Namba za ndugu zao sizijui, hata shem aloondoka Moro asubuhi sikuwa na namba yake bado. Doto ndo analia tu, hata password nitamuombaje? Hanielewi. Nikabidi niunge dakka tu faster nikampigia kaka Hans, nikamuomba atujie maana hakuna wa kuendesha gari. Mimi na wenzangu wamechanganyikiwa afu mimi sijui vizur kuendesha.
0 Comments