
SAUTI YA KIMYA. SEHEMU YA 04. Mwandishi: Chief na simulizi zake WhatsApp: 0621045997 Siku zilivyozidi kusonga mbele, urafiki kati ya Gavin na Allan ulizidi kushika kasi ya ajabu. Gavin, ambaye hapo awali alionekana kama simba asiyekaribika, aligeuka kuwa kivuli cha Allan. Kila mara baada ya vipindi, Gavin alimfuata Allan na kuanza kumsimulia habari za maisha ya nyumbani kwao kuhusu upweke alionao kwenye jumba lao la kifahari, shinikizo kubwa analopata kutoka kwa wazazi wake ili afanye vizuri kimasomo, na jinsi anavyokosa watu wa dhati wa kuongea nao. Alimwamini Allan kiasi cha kufungua moyo wake mzima bila kuficha kitu. Hata hivyo, nje
0 Comments